• HABARI MPYA

  Tuesday, March 10, 2009

  AMBANI AREJEA, AIWEKEA NADHIRI AHLY

  Ambani hapa akiwa kwenye mitaa ya jiji la Zheijang, maskani ya Greentown
  Ambani hapa akifanya mazoezi na wachezaji wa Greentown

  Ambani katika mechi yake ya kwanza aliyoichezea Greentown, hapa anarejea chumba cha kubadilishia nguo baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza


  Ambani akicheza na wachezaji wa Greentown

  MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Mkenya Boniphace Ambani amesema kwamba amerejea akiwa fiti kupita maelezo na sasa anaelekeza nguvu zake katika mchezo dhidi ya Al Ahly ya Misri, Jumapili hii Uwanja wa international mjini Cairo.
  Akizungumza na bongostaz leo mjini Dar es Salaam jana, Ambani aliyetua nchini juzi jioni, alisema kwamba kufanya majaribio na klabu ya Greentown ya Zheijang, China kumemuongezea vitu vingi vya kiufundi ambavyo atavitumia kwenye mechi dhidi ya Ahly.
  “Nashukuru niimefika hapa salama, naamini kabisa nitaisaidia timu yangu kufanya vizuri, huu utakuwa mchezo mgumu, lakini sisi pia tuna timu nzuri na tutapigana kiume,”alisema Ambani.
  Ambani alisema ameiona Yanga ilivyocheza na Vancouver Whitecaps ya Canada jana na kwamba iko vizuri na inaweza kabisa kuisimamisha Ahly kwao. Ambani anatarajiwa kuanza mazoezi na wenzake kesho, Uwanja wa Uhuru, zamani Taifa, Dar es Salaam tayari kwa safari ya keshokutwa kuelekea Cairo kumenyana na Mabingwa wa Afrika mara sita, Ahly katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza, Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Akiwa China kwa majaribio ambako amefuzu, Ambani alicheza mechi mbili za kirafiki, wa kwanza akifunga bao la kwanza dakika ya pili wakati timu yake inashinda 3-2 na wa pili akifunga pia bao la kwanza dakika ya nne, wakati timu yake hiyo inafungwa 3-2.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMBANI AREJEA, AIWEKEA NADHIRI AHLY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top