• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 09, 2009

  MISS UTALII MWANZA KUMEKUCHA


  HATIMAYE ile zara ya warembo wa Taifa wa Miss Utalii Tanzania,ya kuvumbua na kutangaza vivutio vya utalii,utamaduni na utalii wa ndani,imeshika kasi mkoani Mwanza.
  Ziara hiyo inayo jumuisha washindi na washiriki wa fainali za Taifa wa mwaka 2008,na kupewa jina la Miss Tourism –Tanzania Great Safari & Tour 2008 ,mwishoni mwa wiki hii warembo hao watafanya onyesho kubwa na la kihistoria la mavazi katika ukumbi wa Yun Long Chinise Restaurant ,ambao zamani ulikuwa ukijulikana kama Rock Beach Hotel siku ya jumamosi tarehe 14-3-2009 kuanzia saa 2 usiku,na siku ya jumapili tarehe 15-3-2009 onyesho maalum litafanyika ,katika uwanja wa CCM Kirumba kuanzia saa 8 mchana kwaajili wakazi wa Mwanza ambao kwa sababu mbalimbali hawawezi kutoka usiku wakiwemo wanafunzi na watoto.
  Katika onyesho hilo warembo wataonyesha mavazi na vipaji vya kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za makabila yote ya Tanzania.Mavazi yatakayoonyeshwa ni pamoja nay a Asili,Kutokea,Ubunifu na ya kitanzania,ambayo yatakuwa yamebuniwa na wabunifu wakubwa na wakimataifa wakiwemo Chris Design na Kita Design wa jijini Mwanza.
  Aidha msanii mkongwe na wa kimataifa Jita Man aka Zagamba Mamba ataongoza kundi la wanamuziki na wasani wa kitanzanika ambao watakuwa wakichuana na wanamuziki wa kutoka Uganda,ikiwa ni sehemu ya kupamba zaidi onyesho hilo.Pia watakaohudhuria onyesho hilo watajionea na kuburudia pia na kongoma za asili za kadogoli na gobogobo za asili ya kisukuma.
  Warembo wote wapo katika maandalizi makali na mazoezi katika hoteli za kitalii Isamilo Lodge na Midland Hotel za jijini Mwanza.
  Kampuni ya Nyanza Bottling ambao ni mmoja wa wazamini watatoa cocakola ya kopo na maji ya Dasani kwa kila atakaye nunua tiketi ya shilingi 2000 katika onyesho la uwanjani CCM Kirumba,ambapo kiingilio kwa wakubwa ni shilingi 2000 na kwa watoto ni shilingi 1000.New Mwanza Hotel na Midland Hotel wamedhamini ziara hiyo kwa kutoa malazi na chakula kwa warembo pia ukumbi
  Katika onyesho la tarehe 14-3-2009 usiku litakalofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Yun Long Chinise Restaurant zamani Rock Beach Hotel,kwa kila atakaye nunua tiketi ya dhahabu atapata bia moja kutoka kwa kampuni ya Serengeti Breweris ambao ni moja ya wadhamini wa ziara hiyo itakayo wafikisha warembo hao wa Miss Utalii Tanzania katika mikoa yoteTazania bara na visiwani,kiingilio katika onyesho hilo la usiku ni shilingi 10,000 kwa viti vya dhahabu na shilingi 5,000 kwa viti vya shaba.
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mheshmiwa Nsekela anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika onyesho hilo,ambalo pia limdhaminiwa na kituo cha televisheni cha Star TV,Isamilo Lodge,Chris Designe,Kita Designe,Mabasi ya Mombasa Raha,New Age Communication na TANAPA.
  Kabla ya onysho hilo,warembo wote watakwenda kutembelea hifadhi za Taifa za Rubondo na Saanane,pia watatembelea kijiji cha makumbusho cha kisukuma cha Bujora na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kuhamasisha vita dhidi ya mila potofu zikiwemo za mauaji ya albino,tohara kwa wanawake,mauaji ya vikongwe,baguzi wa kijinsia,uharibifu wa mazingira ,uvuvi haramu na uwindaji haramu.
  Maonyesho haya ya mavazi na ziara nzima ya Miss Tourism –Tanzania Great safari & Tour ni fulsa ya pekee kwa watanzania kuhamasishwa juu ya kujenga tabia ya kutembelea vivutio vyetu vya utalii na kuthamini mila,desturi na tamaduni zetu watanzania
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MISS UTALII MWANZA KUMEKUCHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top