• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 12, 2009

  BUNU APIGA NNE, JKT YAILAZA VILLA 5-1

  MSHAMBULIAJI Hussen Bunu alifunga mabao manne peke yake wakati JKT Ruvu ilipoichakaza Villa Squad 5-1 mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa jana katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Ijumaa, Machi 13.
  Wanajeshi hao walianza kuwapeleka mchamcha Villa Squad na kufanikiwa kupata bao la kwanza dakika 13 lilofungwa na Haruna Adolf akiunganisha krosi ya Amos Mgisa.
  Dakika saba baadaye mshambuliaji Hussen Bunu alifungua karamu yake ya mabao kwa kuungasha vema krosi ya Amos Mgisa katika kipindi chote cha kwanza Villa Squad walionekana kuzidiwa kila idara.
  Mambo yalizidi kuwa mabaya kwa vijana hao wa Kinondoni katika kipindi cha pili wakishudia nyota wa mchezo Hussen Bunu akipachika mabao tatu peke yake katika dakika ya 47, 71 na 86.
  Mkongwe Idd Moshi alifunga bao la kufutia macho kwa Villa dakika ya 76 katika mchezo huo uliokuwa wa upande moja. Kwa matokeo hayo JKT Ruvu imepaa kutoka nafasi ya sita hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi 24 kabla ya mechi za leo na kesho, huku Villa Squad na pointi 14 ikizidi kulekezwa njia ya kushuka daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BUNU APIGA NNE, JKT YAILAZA VILLA 5-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top