• HABARI MPYA

  Friday, March 20, 2009

  OWINO, AMBANI MWALALA WAFUATA MAKALI NYUMBANI

  WACHEZAJI wa kimataifa wa Kenya wanaochezea klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Ben Mwalala, Boniphace Ambani, na George Owino waliondoka Jumamosi mjini Dar es Salaam kwenda kwao, Nairobi, Kenya kujiunga na timu yao ya taifa.
  Akizungumza na DIMBA siku hiyo mjini Dar es Salaam, mmoja wa wachezaji hao, Mwalala alisema kwamba wanakwenda kuitikia wito wa kocha mpya wa timu yao ya taifa, Harambee Stars, Mjerumani Antoine Hey anayeianda timu hiyo na mchezo dhidi ya Tunisia, Machi 28 mwaka huu.
  Wengine aliowaita ni kiungo Osborn Monday na mshambuliaji Francis Ouma wanaochezea klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam pia.
  Mbali na Wakenya hao, beki wa kimataifa wa Malawi, Wisdom Ndhlovu, naye anatarajiwa kurejea nyumbani kujiunga na timu ya taifa ya kwao, kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010.
  Wachezaji wote hao wanatakiwa kurudi Dar es Salaam mara tu baada ya mechi hizo, ili kuungana na Yanga kujiandaa na mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya Al Ahly ya Misri Aprili 5, mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OWINO, AMBANI MWALALA WAFUATA MAKALI NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top