• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 17, 2009

  KONDIC AKATA TAMAA, ATUNISHIANA MSULI NA WAKILI WA TFF


  Na Majuto Omari, Cairo
  MKUU wa msafara wa wa Yanga, Alex Mgongolwa na kocha mkuu wa klabu hiyo, Dusan Kondic wametupiana maneno baada ya Mserbia huyo kuonyesha kukata tamaa baada ya kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Al Ahly.
  Katika mchezo huo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Cairo, Yanga ililala kwa kujitengenezea deni la mabao 4-0 katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo.
  Baada ya kipigo hicho, Kondic aliueleza uongozi kuwa hali ni ngumu katika mchezo ujao jijini Dar es Salaam, jambo ambalo lilifanya wakili Mgongolwa kuhamaki na kumwambia, ìhaiwezekani wewe kama kocha useme maneno hayo, wachezaji nao watasema nini.î
  Hata hivyo, baada ya kupishana kauli, hali hiyo iliwekwa sawa na viongozi wengine waliomo katika msafara huo huku mwenyekiti wa Yanga, Iman Madega akiingilia kati na kusema kuwa mchezo wa marudiano utakuwa mgumu.
  "Tungeweza kujiandaa zaidi, lakini ratiba ya Ligi Kuu itakuwa inatukwaza, tuna mechi na Toto Afrika ya Mwanza na baadaye mechi mfululizo za Dar es Salaam, hizo zitatuvuruga tungetaka muda mrefu wa maandalizi," alisema.
  Mbali na maneno hayo, wachezaji kwa nyakati tofauti, walilalamikia programu ya mazoezi ya timu hiyo kabla ya kurudiana na Waarabu hao.
  Baadhi yao, Ben Mwalala, Mrisho Ngassa, Athumani Idd 'Chuji' na Nurdin Bakari waliiambia Mwananchi kwa nyakati tofauti kuwa kama kungekuwa na maandalizi ya maana, Al Ahly ni wepesi wangeweza kuiondoa.
  Wachezaji hao waliokuwa timu ya taifa iliyoshiriki fainali za Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) walitaka kupewa mazoezi ya nguvu.
  Beki Nadir Haroub ëCannavaroí alisema kuwa wakiweza kujituma na kucheza kwa nguvu, wanao uwezo wa kupata mabao mabao matatu na zaidi.
  "Tunaweza kuwamudu, tufanye mazoezi na kujipanga, tutashinda huko kwetu," alisema.
  Yanga inararajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam leo saa 3:00 asubuhi ikitokea Cairo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KONDIC AKATA TAMAA, ATUNISHIANA MSULI NA WAKILI WA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top