KLABU ya Simba imevunja mkataba na wachezaji wengine wawili, kiungo Abdulsamad Kassim Ali na winga Mmalawi, Duncan Nyoni ambao wote walisajiliwa mwanzoni mwa msimu, Agosti mwaka jana.
Wawili hao wanafanya idadi ya wachezaji walioachwa Simba kufika watatu baada ya kiungo mwingine mzawa, Ibrahim Ajibu Migomba aliyehamia Azam FC.
Aisha, Wekundu hao wa Msimbazi wamemtoa kwa mkopo kipa Jeremiah Kisubi kwenda Mtibwa Sugar hadi mwishoni mwa msimu. Kasubi pia alisajiliwa mwanzoni mwa msimu kutoka Tanzania Prisons.
0 comments:
Post a Comment