• HABARI MPYA

  Tuesday, January 04, 2022

  KMKM YASHINDA, MLANDEGE YATOA DROO MAPINDUZI


  TIMU ya KMKM imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Taifa Jang'ombe mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi B usiku wa Jumatatu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mabao ya KMKM yamefungwa na Eliasa Suleiman dakika ya 34 na la penalti la Abrahman Othman dakika ya 45 na ushei, wakati la Taifa limefungwa na Yasir Masoud dakika ya 40.
  Mechi iliyotangulia ya Kundi C baina ya Selem View na Mlandege ilimalizika kwa sare ya bila mabao.
  Michuano hiyo itaendelea Jumanne kwa mechi mbili pia, Namungo na Yosso Boys Saa 10:05 jioni na Azam FC dhidi ya Meli 4 City Saa 2:15 usiku zote za Kundi A hapo hapo Uwanja wa Amaan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMKM YASHINDA, MLANDEGE YATOA DROO MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top