• HABARI MPYA

  Thursday, December 03, 2020

  TANZANIA YATOA MCHEZAJI BORA NA MFUNGAJI BORA WA MICHUANO YA CECAFA U20 ARUSHA 2020

   

  PAMOJA na kupokonywa Kombe la CECAFA U20 kufuatia kipigo cha 4-1 kutoka kwa Uganda jana wa Uwanja wa Black Rhino Academy, Karatu mkoani Arusha – Ngorongoro Heroes imetoa Mchezaji Bora na Mfungaji Bora wa Mashindano hayo yaliyofikia tamati jana.

  Hao ni Abdul Suleiman (chini) aliyetwaa Kiatu cha Rangi ya Dhahabu kwa mabao yake matano akifungana  na Ivan Bogere wa Uganda na Paschal Mshindo (juu) aliyetwaa Mpira wa rangi ya Dhabau, wakati Kipa Bora ni wa Sudan Kusini.

  Uganda na Tanzania zitacheza AFCON U20 itakayofanyika Mauritania kuanzia Februari 14 hadi Machi 4 mwakani.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YATOA MCHEZAJI BORA NA MFUNGAJI BORA WA MICHUANO YA CECAFA U20 ARUSHA 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top