• HABARI MPYA

  Wednesday, December 09, 2020

  RONALDO APIGA MBILI JUVE YAICHAPA BARCA 3-0 CAMP NOU


  Cristiano Ronaldo wa Juventusn(kushoto) na Lionel Messi wa Barcelona (kulia) wakizungumza wakati wa mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou. Juventus ilishinda 3-0, Ronaldo akifunga mabao mawili yote kwa penalti dakika ya 13 na 52 na kufikisha jumla ya mabao 134 kwenye michuano hiyo, wakati bao lingine lilifungwa na Weston McKennie dakika ya 20, huku kipa mkongwe wa umri wa miaka 42, Gianluigi Buffon akijizlea sifa kwa kuokoa michomo mingi ya hatari ya Messi. Timu hizo zote zimemaliza na pointi 15 kila moja na kutinga pamoja 16 Bora, Juve wakiwa juu ya Barcelona kutokana na ushindi wao wa jana
   

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO APIGA MBILI JUVE YAICHAPA BARCA 3-0 CAMP NOU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top