• HABARI MPYA

  Wednesday, December 09, 2020

  MAN UNITED WAPIGWA 3-2 NA KUTUPWA NJE LIGI YA MABINGWA


  Mshambuliaji Mholanzi Justin Kluivert (kulia) akishangilia baada ya kuwafungia RB Leipzig bao la tatu dakika ya 69 katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Manchester United kwenye mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Red Bull Arena, Leipzig. Mabao mengine ya RB Leipzig yalifungwa na Angelino dakika ya pili na Amadou Haidara dakika ya 13, wakati ya Manchester United  yalifungwa na Bruno Fernandes dakika ya 80 kwa penalti na Ibrahima Konate aliyejifunga dakika ya 82 baada ya kazi nzuri ya Paul Pogba. Kwa matokeo hayo, Man United wanatolewa Ligi ya Mabingwa na kuhamia Europa League, wakati RB Leipzig inasonga mbele pamoja na PSG
   

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED WAPIGWA 3-2 NA KUTUPWA NJE LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top