• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 08, 2020

  DK MSOLLA AWATEUA MAWAKILI WATANO KUUNDA KAMATI NDOGO YA MABADILIKO YANGA SC

  MWENYEKITI wa Yanga SC, Dk Mshindo Msolla kwa kushirikiana na Kamati yake ya Utendaji, amewateua wanachama wanane kuunda Kamati Ndogo ya Mabadiliko, ambao ni (Mwenyekiti) Wakili Raymond Wawa na Wajumbe; Wakili Sam Mapande, Wakili Audats Kahendagile, Wakili Imani Madega, Wakili Mark Anthony, Mohammed Msumi, Pastory Kyombya na Deborah Mkemwa.

  Kamati Kuuya Mabadiliko ya Yanga SC inaundwa na Mwenyekiti, Wakili Alex Mgongolwa na Wajumbe; Profesa Mgongo Fimbo, mtaalam wa katiba na sheria za ardhi, Said Meckisadiki - mkuu wa mkoa mstaafu, Mohamed Nyenge, Mchumi, George Fumbuka, Mshauri masuala ya uwekezaji na Felix Mlaki - mchumi na mtaalam wa masuala ya fedha.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DK MSOLLA AWATEUA MAWAKILI WATANO KUUNDA KAMATI NDOGO YA MABADILIKO YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top