• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 05, 2020

  MESSI AFUNGA PENALTI BARCA YAIPIGA DYNAMO KIEV 2-1 NYUMBANI


  Nahodha wa Barcelona, Lionel Messi akishangilia kwa staili yake maarufu baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza kwa penalti dakika ya tano katika ushindi wa 2-1 dhidi ya FC Dynamo Kyiv kwenye mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou. Bao la pili la Barcelona lilifungwa na Gerard Pique dakika ya 65, kabla ya Viktor Tsygankov kuwafungia bao la kufutia machozi wageni dakika ya 75. Kwa ushindi huo, Barcelona inafikisha pointi tisa na kuendelea kuongoza kundi kwa pointi tatu zaidi ya Juventus inayofuatia baada ya kila timu kucheza mechi tatu
   

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI AFUNGA PENALTI BARCA YAIPIGA DYNAMO KIEV 2-1 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top