• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 05, 2020

  MORATA APIGA MBILI JUVENTUS YAUA 4-1 UGENINI ULAYA


  Alvaro Morata akishangilia baada ya kuifungia Juventus mabao mawili dakika ya saba na 60 katika ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Ferencvaros kwenye mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Puskas Arena Jijini Budapest, Hungary. Mabao mengine ya Juve yalifungwa na Paulo Dybala dakika ya 72 na Lasha Dvali aliyejifunga dakika ya 81, wakati la Ferencvaros la kufutia machozi lilifungwa na Franck Boli dakika ya 90 na ushei na kwa ushindi huo, Kibibi Kizee cha Turin kinafikisha pointi sita na kupanda nafasi ya pili kwenye kundi kikizidiwa pointi tatu na vinara, Barcelona baadaya timu zote kucheza mechi tatu
   

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MORATA APIGA MBILI JUVENTUS YAUA 4-1 UGENINI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top