• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 02, 2020

  WAAMUZI LIGI KUU WALIPWA SH. MILIONI 555 MALIMBIKIZO YA MALIPO YAO WALIYOKUWA WANAIDAI TFF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BODI ya Ligi Tanzania (TPLB) kwa pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wamelipa kiasi cha 555,661, 400 kwa waamuzi wa Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na la Pili Tanzania Bara.
  Taarifa ya Bodi ya Ligi imesema; “Tunakwenda kuanza ligi wakati hakuna Mwamuzi anayedai msimu huu.”.
  Hatua hiyo inakuja siku moja tu baada ya Bodi ya Ligi kutoa ratiba ya mechi za viporo za Ligi Kuu baada ya mapumziko ya miezi miwili na ushei kufuatia mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 19.
  Rais wa TFF, Wallace Karia akipokea msaada wa vitakasa mikono na Barakoa kutoka kwa Mkurugenzi wa KIDC, Dar es Salaam, Goners Kim 

  Kwa msimu wote huu kumekuwa na malalamiko ya marefa kutolipwa fedha zao kwa muda mrefu na ingawa awali TFF ilikuwa inakana madai hiyo – lakini ilifikia wakati ikakiri na kabla ya taarifa hii ya ulipaji.
  Ligi Kuu inatarajiwa kuanza tena Jun 13 baada ya kusimama tangu Machi 17, mwaka huu TFF kwa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufuatia mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa corona duniani kote.  
  Ligi Kuu ilisimama huku Simba SC ikiwa inaongoza kwa pointi zake 71, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 54 baada ya timu zote kucheza mechi 28, wakati vigogo, Yanga SC ni wa tatu kwa pointi zao 51 za mechi 27 na Namungo wa nne wakiwa na pointi 50 za mechi 28.
  Hali ni mbaya kwa Singida United inayoshika mkia kwa pointi zake 15 za mechi 29, nyuma ya Mbao FC pointi 22 mechi 28, Alliance FC pointi 29, mechi 29, Mbeya City pointi 30 mechi 29 na Ndanda FC pointi 31 mechi 29.
  Wakati huo huo: Rais wa TFF, Wallace Karia amepokea msaada wa vitakasa mikono na Barakoa kutoka kwa Mkurugenzi wa KIDC Jijini Dar es Salaam, Goners Kim zitakazosaidia kujikinga na virusi vya corona.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WAAMUZI LIGI KUU WALIPWA SH. MILIONI 555 MALIMBIKIZO YA MALIPO YAO WALIYOKUWA WANAIDAI TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top