• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 14, 2020

  BARCELONA WAREJEA KWA KISHINDO LA LIGA, WAICHAPA MALLORCA 4-0

  Lionel Messi akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia Barcelona bao la nne dakika ya 90 na ushei katika ushindi wa 4-0 dhidi ya wenyeji, Mallorca kwenye mchezo wa LaLiga usiku wa jana Uwanja wa Iberostar. Mabao mengine ya Barcelona yamefungwa na Arturo Vidal dakika ya pili, M. Braithwaite dakika ya 37 na Jordi Alba dakika ya 79 na sasa Barca inafikisha pointi 61 katika mchezo wa 28 ikiendelea kuongoza La Liga kwa pointi tano zaidi ya Real Madrid ambayo leo inamenyana na Eibar 
    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BARCELONA WAREJEA KWA KISHINDO LA LIGA, WAICHAPA MALLORCA 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top