• HABARI MPYA

    Sunday, June 14, 2020

    SIMBA SC YAPUNGUZWA KASI LIGI KUU, YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA RUVU SHOOTING LEO TAIFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MABINGWA watetezi, Simba SC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
    Kwa sare hiyo, Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Sven Ludwig Vandenbroeck anayesaidiwa na mzawa Suleiman Matola inafikisha pointi 72 katika mchezo wa 29, ikiendelea kuongoza Ligi Kuu kwa ponti 18 zaidi ya Azam FC na Yanga zinazofuatia baada ya zote kucheza mechi 28 pia.
    Katika mchezo wa leo, Simba SC ilitangulia kwa bao la kiungo wake Shiza Ramadhani Kichuya dakika ya 12 akimalizia mpira uliorudi baada ya kuokolewa na kipa wa Ruvu Shooting, Mohamed Makaka kufuatia shuti lake mwenyewe awali akimalizia krosi ya mshambuliaji Mnyarwanda, Medie Kagere.

    Mshambulaji mkongwe, Fully Zulu Maganga akaisawazishia Ruvu Shooting inayofundishwa na Salum Mayanga dakika ya 37 akimalizia pasi ya Abdallahman Mussa kumtungua kipa namba moja Tanzania, Aishi Salum Manula.
    Baada ya hapo, timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu hususan kipindi cha pili baada ya makocha wote kufanya mabadiliko ya wachezaji kadhaa, lakini matokeo hayakubadilika.
    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gardiel Michael/Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ dk68, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Muzamil Yassin, Hassan Dilunga/Deo Kanda dk68, Luis Miquissone/Miraji Athumani dk82, Medie Kagere, John Bocco na Shiza Kichuya/ Francis Kahata dk61.
    Ruvu Shooting; Mohamed Makaka, Omary Kindamba, Kassim Simbaulanga, Rajab Zahir, Baraka Mtuwi, Zuberi Dabi, Abdulrahman Mussa/Said Dilunga dk79, Shaaban Msala, Graham Naftal/Moses Shaaban dk79, Fully Maganga/Sadat Mohamed dk70 na William Patrick/Jamal Mnyate dk63.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAPUNGUZWA KASI LIGI KUU, YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA RUVU SHOOTING LEO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top