• HABARI MPYA

  Friday, June 12, 2020

  WAKUFUNZI WA CAF NA FIFA WAIPA AZAM FC MWONGOZO WA KUIENDESHA TIMU YAO KIUWELEDI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Azam FC unaendelea na mchakato wa kufanikisha uendeshaji wa timu katika misingi ya kiuweledi.
  Mchakato huo unaratibiwa na Wakufunzi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na Afrika (CAF), Dr. Henry Tandau (Utawala, FIFA) na Sunday Kayuni (Makocha, CAF).
  Wakufunzi hao jana waliwasilisha uchambuzi wa mchakato huo, mara baada ya kufanya tathimini ya awali, iliyohusisha mahojiano yao binafsi waliofanya na wachezaji, makocha, wafanyakazi na watu wa karibu na eneo la makao makuu ya klabu, Azam Complex.
  Mara baada ya kuwasilisha uchambuzi huo, wakufunzi hao wataandaa mafunzo kwa idara mbalimbali ndani ya timu hiyo kuanzia kwenye uongozi, wafanyakazi, makocha, wachezaji na idara ya habari.
  Aidha baada ya mafunzo hayo, mchakato huo utahitimishwa na utekelezaji wa kila idara katika shughuli zao za kila siku za klabu, wakitakiwa kuhakikisha wanatimiza kiuweledi yale yote waliyofundishwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAKUFUNZI WA CAF NA FIFA WAIPA AZAM FC MWONGOZO WA KUIENDESHA TIMU YAO KIUWELEDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top