• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 26, 2020

  CHELSEA WAIPIGA MAN CITY 2-1 NA KUIPA UBINGWA LIVERPOOL

  Willian akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia Chelsea bao la pili kwa penalti dakika ya 78 ikiilaza Manchester City 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja Stamford Bridge, London. Bao la kwanza la Chelsea lilifungwa na Christian Pulisic dakika ya 36 kabla ya Kevin De Bruyne kuisawazishia Man City dakika ya 55 ambayo ilimaliza pungufu kufuatia Fernandinho kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 77 kwa kuchez rafu. Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 54 baada ya kucheza mechi 31, ingawa inabaki nafasi ya nne nyuma ya Leicester City wenye pointi 55, Manchester City pointi 63 na Liverpool pointi 86 ambao sasa ni mabingwa rasmi wa England baada ya maka 30 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA WAIPIGA MAN CITY 2-1 NA KUIPA UBINGWA LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top