• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 15, 2020

  REAL MADRID YARUDI NA MOTO LA LIGA, YAICHAPA EIBAR 3-1

  Wachezaji wa Real Madrid wakimpongeza mwenzao, Toni Kroos baada ya kumtungua kipa Marko Dimitrovic kuifungia timu yake bao la kwanza dakika ya nne katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Eibar kwenye mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Alfredo Di Stefano Jijini Madrid. Mabao mengine ya Real Madrid yalifungwa na Nahodha Sergio Ramos dakika ya 30 na Marcelo dakika ya 37, wakati bao pekee la Eibar lilifungwa na Pedro Biga dakika ya 60 na kwa ushindi huo kikosi cha Mfaransa, Zinedine Zidane kinafikisha pointi 59 katika mchezo wa 28, kikiendelea kuzidiwa pointi mbili na vinara na mabingwa watetezi,  Barcelona baada ya wote kucheza mechi 28PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL MADRID YARUDI NA MOTO LA LIGA, YAICHAPA EIBAR 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top