• HABARI MPYA

  Monday, June 15, 2020

  YANGA SC YAACHANA NA KATIBU MKUU WAKE, DK DAVID LUHAGO WAKILI SIMON PATRICK KUKAIMU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Yanga SC imefikia uamuzi wa kuachana na Katibu Mkuu wake, Dk David Luhago baada ya makubaliano naye leo Jijini Dar es Salaam na nafasi yake itakaimiwa na Wakili Simon Patrick.
  Taarifa ya Yanga SC leo imesema kwamba makubaliano hayo yamefikiwa baada ya majadiliano ya pande zote mbili – yaani uongozi na Luhago kwa maslahi mapana ya klabu na kwa sasa Wakili Patrick ambaye ni Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama atakaimu nafasi hiyo.
  “Uongozi wa klabu ya Yanga na Katibu Mkuu, David Luhago na Katibu Mkuu, David Luhago leo tarehe 15/06,2020 umefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa ajira wa Katibu Mkuu,”imesema taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo.
  Dk David Ruhago (walioketi kulia), akiwa na Mkurugenzi wa Mashindano Thabit Kandoro. Wengine waliosimama ni kutoka kulia Hassan Bumbuli, Mkurugenzi wa Masoko na Biashara, Robert Kabeya Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama,  Simon Patrick.

  Uongozi wa Yanga SC chini ya Mwenyekiti, Dk. Mshindo Msolla ulimtangaza rasmi Luhago kuwa Katibu Mkuu mpya Novemba 11 mwaka jana, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Charles Boniface Mkwasa ambaye kwa sasa ni Kocha Msaidizi wa klabu.
  Ruhago aliajiriwa kwa pamoja na Mkurugenzi wa Mashindano Thabit Kandoro, Mkurugenzi wa Masoko na Biashara, Robert Kabeya, Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama,  Simon Patrick na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilian, Bumbuli.
  Kwa mwaka mzima baada ya kuondoka kwa Mkwasa, nafasi ya Kaimu Katibu Mkuu Yanga SC ilikaimiwa na viongozi watatu tofauti ambao ni Omar Kaya, Dismas Ten na Thabit Kandoro aliyekaimu nafasi hiyo kwa siku 11 tu tangu Novemba 1, mwaka jana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAACHANA NA KATIBU MKUU WAKE, DK DAVID LUHAGO WAKILI SIMON PATRICK KUKAIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top