• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 14, 2020

  WAFANYAKAZI WA AZAM FC WAWAFUNDISHA KABUMBU 'MABOSI' WA TFF, WAWACHAPA 4-0 KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya wafanyakazi wa Azam FC imefanya kweli baada ya kuwafunza soka wafanyakazi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikiwanyuka mabao 4-0.
  Mechi hiyo ya kirafiki ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili.
  Wafanyakazi wa Azam FC walionyesha umwamba mkubwa wa kutandaza soka kwa dakika zote 90 za mchezo huo.
  Mabao ya washindi yaliwekwa kimiani na John Matambara, aliyefunga mara mbili huku Victor Ndozero na Feisal wakitupia mengine.

  Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza ya wafanyakazi wa Azam FC, tokea timu hiyo iundwe, na mafanikio yamekuwa makubwa sana.
  Mapema kabla ya mechi hiyo, Azam FC walitekeleza kwa vitendo siku ya wachangiaji damu duniani, kwa baadhi ya wafanyakazi wake kuchangia damu kwenye benki ya Taifa ya Damu Salama.
  Zoezi hilo lilifanyika kwenye viunga vya Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na watu wengine mbalimbali wakiwemo mashabiki wa soka, waliruhusiwa kuchangia damu.
  TFF kwa kushirikiana na Azam FC wamedhamini zoezi hilo, lengo likiwa ni kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa damu hospitalini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WAFANYAKAZI WA AZAM FC WAWAFUNDISHA KABUMBU 'MABOSI' WA TFF, WAWACHAPA 4-0 KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top