• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 17, 2020

  AZAM FC YATHIBITISHA KUACHANA NA DONALD NGOMA BAADA YA MIAKA MIWILI YA KUWA NAYE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam imethibitisha kuachana rasmi na aliyekuwa mshambuliaji wake, Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma, baada ya mkataba wake kufikia ukingoni Juni 14 mwaka huu.
  “Baada ya makubaliano ya pande zote mbili, hatimaye kila upande umekubaliana kutoendelea na nyongeza ya mkataba mpya baada ya ule wa awali kufikia ukingoni,”.
  “Tunathamini mchango wake wote alioutoa kwenye klabu yetu, kwa kufunga mabao yaliyosaidia kuchukua mataji mawili, Kombe la Mapinduzi mwaka jana na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) msimu uliopita,” imesema taarifa ya Azam FC.
  Kwa kipindi chote cha misimu miwili, alichodumu ya Azam FC, Ngoma amekuwa mmoja ya washambuliaji wa kutumainiwa akiwa mfungaji bora wa timu yetu msimu uliopita kwa mabao yake 14 aliyoifunga kwenye mashindano yote.
  Hadi anamaliza mkataba wake kwenye timu hiyo yenye maskani yake Azam Complex, Chamazi, Ngoma amefanikiwa kucheza jumla ya mechi 42 za mashindano yote, akihusika katika mabao 20, baada ya kufunga 16 na kutoa pasi za mwisho nne.
  “Tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya ya soka, popote atakapoenda. Asante sana Donald Ngoma,” imesema taarifa hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YATHIBITISHA KUACHANA NA DONALD NGOMA BAADA YA MIAKA MIWILI YA KUWA NAYE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top