• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 17, 2020

  BERNARD MORRISON KUJIUNGA NA WENZAKE YANGA SC TIMU ITAKAPOREJEA KUTOKA DODOMA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO mshambuliaji wa Yanga SC, Bernard Morrison atajiunga na wenzake mara kikosi kitakaporejea Dar es Salaam kesho kutoka Dodoma.
  Yanga SC leo wanatarajiwa kuwa wageni wa JKT Tanzania katika mchezo wa kiporo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Na Morrison hakusafiri na wenzake wiki iliyopita kwa mechi mbili za ugenini, ikiwemo na ile waliyoshinda 1-0 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Kambarage kutokana na kuwa mejeruhi.
  Bernard Morrison (kushoto) akiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga SC, Wakili Simon Patrick (katikati) makao makuu ya klabu, Jangwani jana

  Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga SC, Wakili Simon Patrick amesema kwamba jana alifanya mazungumzo na Morrison makao makuu ya klabu, Jangwani na kukubaliana kesho ajiunge na timu.
  Na Patrick ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama atakaimu nafasi hiyo alifanya hayo siku moja tu baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya Dk David Luhago aliyeondolewa kazini baada ya majadiliano ya pande zote mbili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BERNARD MORRISON KUJIUNGA NA WENZAKE YANGA SC TIMU ITAKAPOREJEA KUTOKA DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top