• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 21, 2020

  YANGA SC NA AZAM FC HAKUNA MBABE UWANJA WA TAIFA, ZAMALIZANA KWA SARE YA BILA KUFUNGANA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU za Azam FC na Yanga SC zimegawana pointi moja kila moja baada ya sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
  Ulikuwa mchezo mzuri uliochezeshwa na refa anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Heri Sasii aliyesaidiwa na Soud Lila na Mbaraka Haule wote Dar es Salaam.
  Kwa matokeo hayo, Azam FC inaendelea kushika nafasi ya pili ikifikisha pointi 58, ikiendelea kuizidi  Yanga pointi mbili baada ya wote kucheza mechi 30 sasa.

  Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Sven Ludwig Vandenbroeck inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 75 baada ya kucheza mechi 30.
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Deus Kaseke, Jaffar Mohamed, Kelvin Yondan, Said Juma ‘Makapu’, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Haruna Niyonzima, Mapinduzi Balama/Mrisho Ngassa dk64, Ditram Nchimbi/Abdulaziz Makame dk79, Patrick Sibomana/Bernard Morrison dk46 na David Molinga/Yikpe Gislain dk64. 
  Azam FC; Benedict Haule, Nico Wadada, Salmin Hoza, Abdallah Kheri, Oscar Maasai, Mudathir Yahya, Iddi Kipagwile/Bruce Kangwa dk60, Bryson Raphael, Rochard D’jodi/Andrew Simchimba dk69, Never Tigere/Shaaban Iddi Chilunda dk60 na Iddi Suleiman ‘Nado’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC NA AZAM FC HAKUNA MBABE UWANJA WA TAIFA, ZAMALIZANA KWA SARE YA BILA KUFUNGANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top