• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 03, 2020

  ULIMBOKA MWAKINGWE ARIDHIKA KUFUKUZWA KAZI AFC ARUSHA, SASA ANATAFUTA TIMU NYINGINE

  Na Clement Shari, ARUSHA
  KOCHA Ulimboka Alfred Mwakingwe amesema kwamba ameupokea kwa moyo mweupe uamuzi wa kufukuzwa kazi katika klabu ya AFC Arusha na kwa sasa yupo kwenye mpango wa kujiunga na timu nyingine. 
  Mwakingwe amesema taarifa za yeye kufukuzwa katika timu hiyo alizipata kutoka kwa mmoja wa viongozi wa timu hiyo aliyempigia simu na kumtaarifu kutokuendelea naye na pia kupitia vyombo vya habari.       
  Mwakingwe mshambuluaji wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi Simba amesema alikuwa anafanya kazi ya kujitolea ndani ya AFC kwani alikuwa halipwi kutokana na hali mbaya ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo lakini pia alikuwa hana mkataba.

  Ulimboka Mwakingwe ameupokea kwa moyo mkunjufu uamuzi wa kufukuzwa kazi AFC Arusha

  Amesema kwa sasa maisha yanaendelea kama kawaida na anafanya mazungumzo na mojawapo za klabu zinazoshiriki ligi daraja la kwanza ambayo hakuwa tayari kuitaja huku akidai mazungumzo yanakwenda vizuri.             
  Mei 31 klabu ya AFC Arusha ilitangaza kuachana na aliyekuwa kocha wao mkuu Ulimboka Mwakingwe na nafasi yake kuchukuliwa na Martin Mahimbo atakayekuwa anasaidiwa na Abdallah Juma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ULIMBOKA MWAKINGWE ARIDHIKA KUFUKUZWA KAZI AFC ARUSHA, SASA ANATAFUTA TIMU NYINGINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top