• HABARI MPYA

  Monday, June 22, 2020

  REAL YAICHAPA SOCIEDAD 2-1 NA KUPANDA KILELENI LA LIGA

  Karim Benzema akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid bao la ushindi dakika ya 70 kwa msaada wa VAR katika ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Real Sociedad kwenye mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Reale Arena, au Donostia-San Sebastian. Bao la kwanza la Real Madrid lilifungwa na Nahodha, Sergio Ramos kwa penalti dakika ya 50 wakati la Real Sociedad lilifungwa na Mikel Merino dakakika ya 83. Kwa ushindi huo Real Madrid inafikisha pointi 65, sawa na mabingwa watetezi, Barcelona baada ya wote kucheza mechi 30 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL YAICHAPA SOCIEDAD 2-1 NA KUPANDA KILELENI LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top