• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 22, 2020

  MBWANA SAMATTA ATOKEA BENCHI TENA ASTON VILLA YAPIGWA 2-1 NA CHELSEA NYUMBANI

  Na Mwandshi Wetu, BIRMINGHAM 
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta kwa mara nyngine jana ametokea benchi na kushindwa kuisaidia timu yake, Aston Villa na kipigo cha nyumbani baada ya kuchapwa 2-1 na Chelsea. 
  Samatta aliingia dakika ya 57 kwenda kuchukua nafasi ya Keinan Davis wakati huo tayari Aston Villa wanaongoza 1-0 kwa bao la Kortney Hause dakika ya 43.
  Hata hivyo, akiwa uwanjani – Samatta akashuhudia Chelsea ikitoka nyuma na kupata ushind wa 2-1 kwa mabao ya Christian Pulisic dakika ya 60 na Olivier Giroud dakika ya 62.
  Hali ni mbaya kwa Aston Villa ikibaki na pointi zake 26 baada ya mechi 30 na inaendelea kushika nafasi ya 19 mbele ya Norwich City inayoshika mkia kwa pointi zake 21 za mechi 30 pia wote pamoja na West Ham United na AFC Bournemouth zenye pointi 27 za mechi 30 wakiichungulia vizuri Championship.
  Kikosi cha Aston Villa kilikuwa; Nyland, Konsa, Hause, Mings, Target, McGinn/Jota dk87, Luiz, Hourihane/Nakamba dk70, El Ghazi/Trezeguet dk70, Grealish na Davis/Samatta dk57.
  Chelsea; Kepa, Azpilicueta, Christensen, Rudiger, Alonso, Kante, Kovacic/Barkley dk55, Willian/James dk90, Loftus-Cheek/Pulisic dk55, Mount na Giroud/Abraham dk80.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBWANA SAMATTA ATOKEA BENCHI TENA ASTON VILLA YAPIGWA 2-1 NA CHELSEA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top