• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 27, 2020

  SERIKALI YARUHUSU MASHABIKI KUINGIA KWENYE MECHI YA PRISONS NA SIMBA SC KESHO SOKOINE

  Na Mwandshi Wetu, DAR ES SALAAM
  SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu mashabiki kuingia katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Kati ya Tanzania Prisons na Simba SC kesho Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. 
  Taarifa ya Wizara kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) imesema kwamba hatua hiyo inafuatia ombi la Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya kutaka mechi za Prisons Uwanja wa Sokoine mashabiki waruhusiwe kuingia.  
  Ombi hilo lilifuatia Serikali kuzuia mashabiki kuingia viwanjani katika mechi zote zinazohusu Simba na Yanga nje ya Dar es Salaam baada ya klabu ya kukiuka mwongozo wa wizara ya Afya juu ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona katika mchezo wake dhidi ya Simba SC.
  Simba SC inahitaji sare tu katika mchezo wa kesho ili kutawazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya tatu mfululizo ikiwa imebekiza mechi sita.
  Kwa sasa Simba SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 78 baada ya kucheza mechi 31, ikifuatwa kwa mbali na watani wao wa jadi, Yanga SC wenye pointi 60 za mechi 32, wakati Azam FC yenye pointi 59 za mechi 32 ni ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SERIKALI YARUHUSU MASHABIKI KUINGIA KWENYE MECHI YA PRISONS NA SIMBA SC KESHO SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top