• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 23, 2020

  MTIBWA SUGAR YAWATANDIKA SINGIDA UNITED 3-1, TANZANA PRISONS NA JKT TANZANIA ZATOKA SARE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mtibwa Sugar imepata ushindi wa ugenini wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Singida United jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Liti, zamani Namfua mkoani Singda.
  Mabao ya Mtibwa Sugar leo yamefungwa na Boban Zirintusa dakka ya saba na 25 na Riphat Msuya dakika ya 64, wakati bao pekee la Singida United limefungwa na Ramadhani Hashim dakika ya 87.
  Mwadui FC nayo imeutumia vyema Uwanja wa nyumbani, Mwadui Complex, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga baada ya kuchapa Lipuli FC 3-0, mabao ya Isihaka Kauju aliyejifunga dakika ya 26, Wallace Kiango dakika ya 66 na Omary Dagashenko dakika ya 83.
  Bao pekee la Jordan John dakika ya sita likaipa Mbao FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, wakati Ruvu Shooting imelazimishwa sare ya 0-0 na Ndanda SC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Nayo Tanzania Prisons ikalazimishwa sate ya 2-2 na JKT Tanzania Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Prisons yalifungwa na Adily Buha dakika ya 47, Jeremiah Juma dakika ya 83 na ya JKT yamefungwa na Michael Aidan dakika ya 16 na Mohamed Rashid dakika ya 68.
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mechi nyingine tano; Kagera Sugar na Azam FC Uwanja wa Kaitaba Bukoba, Mbeya City na Simba SC Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Yanga SC na Namungo FC Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Alliance FC na Polisi Tanzania Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza na Biashara United na KMC FC Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAWATANDIKA SINGIDA UNITED 3-1, TANZANA PRISONS NA JKT TANZANIA ZATOKA SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top