• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 08, 2019

  WATANZANA WACHAPWA KWA ‘KNOCKOUTS’ MAPAMBANO YA UTANGULIZI RUIZ NA JOSHUA

  Na Mwandsh Wetu, SYDNEY
  MABONDIA wa Tanzania, Swedi Mohamed na Suleiman Said jana wote walipigwa kwa Knockout (KO) wakipigana mapambano ya utangulizi kabla ya pambano la marudiano baina ya Andy Ruiz Jr. na Anthony Joshua ukumbi wa Diriyah Arena mjini Diriyah nchini Saudi Arabia.
  Swedi Mohamed  alichapwa na Ivan 'Hopey' Price wa Uingereza raundi ya tatu katika uzito wa Super Bantam na Suleiman Said akakaa Raundi ya kwanza mbele ya Mmarekani Diego Pacheco katika uzito wa Middle.
  Muingereza mwenye asili ya Nigeria, Anthony Joshua alifanikiwa kurejesha mataji yake ya WBA, WBO, IBO na IBF baada ya kumshinda kwa pointi za majaji wote, 118-110 mara mbili na 119-109, Mmarekani mwenye asili ya Mexico, Andy Ruiz Jr..
  Joshua alipokonywa mataji yake ya WBA, WBO na IBF baada ya kupgwa na Ruiz Jr. kwa Knockout (KO) raund ya saba Juni 1, mwaka huu ukumbi Madison Square Jijini New York, Marekani
  Ikumbukwe juzi bondia mwingine, Mtanzania, Bruno Melkory Tarimo ‘Vifua Viwili’ alifanikiwa kutwaa taji la IBF International uzito wa Super Feather baada ya kumshinda kwa pointi mwenyeji, Nathaniel May ukumbi wa ICC Exhibition Centre mjini Sydney, Australia.
  Bondia huyo mzaliwa wa Rombo, mkoani Kilimanjaro mkazi wa Bagamoyo, mkoani Pwani alimzidi kwa kiasi kikubwa mpinzani wake huyo kwenye pambano hilo la raundi 10 na haikuwa ajabu kutangazwa mshindi jana. 
  Hilo lilikuwa pambano la 28 kwa Tarimo tangu ajiunge na ngumi za kulipwa Desemba 25, mwaka 2013 akiwa ameshinda mara 25, mara tano kwa Knockouts (KO), amepigwa mara mbili zote kwa KO na droo moja.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WATANZANA WACHAPWA KWA ‘KNOCKOUTS’ MAPAMBANO YA UTANGULIZI RUIZ NA JOSHUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top