• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 08, 2019

  SAMATTA AISAIDIA GENK KUFUTA WIMBI LA MECHI NANE BILA SHINDI, YAICHAPA CERCLE BRUGGE 2-1

  Na Mustafa Mtupa, BRUGGE
  MSHAMBULAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amecheza kwa dakika zote 90 timu yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa ugenini 2-1 dhidi ya Cercle Brugge katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Jan Breydelstadion mjini Brugge.
  Mabao ya Genk yalifungwa na Junya Ito dakika ya 34 na Sander Berge dakika ya70, wakati la lilifungwa na Thibo Somers dakika ya 66.
  Na kwa ushindi huo wa kwanza katika mechi tisa, mabingwa hao watetezi, KRC Genk wanafikisha pointi 25 katika mechi ya 18 na Cercle Brugge inabaki na pointi zake nane za mechi 18 mkiani.

  Kabla ya jana, Genk walicheza mechi nane bila kushinda, wakifungwa ya sita huku nyingine mbili wakitoa sare – baada ya kushinda mara ya mwisho Oktoba 26 dhidi ya Cercle Brugge 1-0. 
  Samatta jana amecheza mechi ya 179 akiwa amefunga mabao 71 katika katika mashindano yote tangu ajiunge na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 139 akiwa amefunga mabao 54, kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi 10,  amefunga mabao mawili, katika Super Cup mechi moja, Ligi ya Mabingwa Ulaya mabao matatu, mechi nne.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Vandevoordt, Maehle, Dewaest, Lucumi, Borges/De Norre dk71, Cuesta, Berge, Ito, Ndongala/Paintsil dk67, Samatta na Onuachu/Bongonda dk61.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AISAIDIA GENK KUFUTA WIMBI LA MECHI NANE BILA SHINDI, YAICHAPA CERCLE BRUGGE 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top