• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 08, 2019

  MIGUU YA ATHUMANI IDDI ‘CHUJI’ INAVYOMSALITI MKWASA YANGA SC

  Na Mustafa Mtupa, DAR ES SALAAM
  IIKUWA ni siku ambayo imepambwa na kijua kikali chenye kutoa jasho kwa mtu yeyote yule ambaye angethubutu kutembea kwa mda huo.
  Hii haikunizuia mimi kujaribu kutembe tembea kwakuwa.waswahili wanasema mguu uliotoka mtume kauombea.
  Katika pita pita zangu ghafla kwenye moja ya kijiwe cha kahawa nikasikia mjadala mkubwa kuhusu namna ambavyo timu ya YANGA inaruhusu saana magoli.
  Nikajaribu kuutafuta ukweli kwenye makabati Ya ubongo wangu na kwa haraka saana nikapata majibu yafuatayo.
  Kwenye ustawi wa timu yeyote duniani lazima kuwe na mtu Anayeitwa Holding midiffilder au kiungo makabaji.

  Huyu ni moja ya pingili ya uti wa mgongo kwenye timu .kwani huyu huifanya safu ya ulinzi kuwa na sherehe ya siku kuu isiyo na kikomo kwani kazi mama ya kiungo huyu ni kukata mirija ya mashambulizi yanayo elekea kwenye safu yake ya ulinzi.
  Yanga wanashida kubwa saana katika eneo hili na hii ndo sababu moja wapo inayopelekea waruhusu saana magoli.
  Mechi ya mwishi ga ligi kocha mkwasa alkamua kumjaribu Ally Sonso ambaye kwangu hakuwa ananiaminisha kwamba anaweza kweli kucheza katika eneo hilo.
  Sonso alionekana kuwa mapungufu makubwa hasa namna ya kuwalinda mabeki wa kati wa yanga.
  Ukiangalia kwenye michezo yao karibia yoote y Ligi kuu msimu huu bado tatizo hili linaendelea kuwasakama vilivyo.
  Papy tshishimbi naye ni kama amesahau kukaa karibu na yondani anaonekana kuanza kuipenda zaidi kazi aliyo lazimishwa na Zahera,ni kama anajaribu kutunza energy yake.makame bado anahitaji kukua namuona kwa siku za usoni.
  Eneo lengine lililonijia kwenye kichwa changu ni safu ya ushambuliaji ya Yanga,ndio unaweza ukashangaa kwanini safu ya ushambuliaji ya Yanga nayo inahusika kwenye tatizo hili?😊
  Kwa kawaida mshambuliaji huwa ana majukumu mengi saana anapokuwa uwanjani.katika mechi yeyote ya mpira wa miguu kuna nyakati mbili.
  Wakati wa kwanza ni pale ambapo timu ina miliki mpira na nyakati ya pili ni pake ambapo timu haina mpira.katika nyakati ya kwanza ndio kazi ya kwanza ya mshambuliaji huwa inatumika.hapa msambuliaji huwa ana focus kwenye kufunga tu.
  Lakini katika nyakati ya pili ni pale ambapo timu haina mpira ama wakatk timu inapokuwa imepokonywa mpira hasa wakati inapokuwa katika eneo la timu pinzani.
  Katika nyakati hizi  ndipo ambapo kazi ya ziada ya mshambuliaji huwa inatumika.kazi ya kuzuia.
  Kunako kikosi cha Yanga huwa sioni kabisa safu yake ya ushambuliji ikifanya kazi hiyo.
  DVD  david molinga amaekuwa mzito saana japo amekuwa anajaribu kufanya kitendo hicho lakini mwili wake unaonekana kumsaliti saana.
  Sydney urikohb huwa sioni akifanya ivyo,Patrick Sibomana, Balama mapinduzi nao ni vivo hivyo tu.mbinu hii huwasaidia saana mabeki wa timu husika kufukia. Mashimo ya space ambazo wameziacha wakati wana shambulia.
  Bado pia Shikalo na metacha mnata hawa nishawishi kwamba wanaweza kuvaa viatu wanavyo vaa.kwa kawaida tunasema miongoni mwa sifa mama ya  kipa bora ni yule ambaye anafanya saves ambazo hatukutegemea kama atafanya.
  Wakati yoote hayo yanaendelea kuniandama kwenye kichwa changu .Hakika nikamkumbuka saana ATHUMAN IDD CHUJI  wakati ule yeye akiwa dimba la chini na Haruna dimba la juu.mwisho nikapata jibu kuwa miguu yake bado ina ihukumu Yanga.
  (Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba +255 687 058 966 au @mtotoWamkulima99 kwenye instagram)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MIGUU YA ATHUMANI IDDI ‘CHUJI’ INAVYOMSALITI MKWASA YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top