• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 02, 2019

  FRANK DOMAYO APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU MSULI WA NYAMA ZA PAJA

  Mwandishi Wetu, DARES SALAAM
  NAHODHA Msaidizi wa Azam FC, Frank Domayo, ameondoka nchini alfajiri ya leo kuelekea jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya tatizo la kuchanika msuli wa nyama ya paja.
  Domayo alipata majeraha hayo, wakati akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Guinea ya Ikweta.
  Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Azam FC imeeleza kuwa matibabu yake yatachukua muda wa siku 10 atakazokuwa huko, yakifanyika kwenye Hospitali ya Vincent Palotti chini ya Dr. Robert Nickolas.

  Katika safari yake, Domayo ameambatana na daktari wa timu, Dkt. Mwanandi Mwankemwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FRANK DOMAYO APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU MSULI WA NYAMA ZA PAJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top