• HABARI MPYA

    Wednesday, May 22, 2019

    TP MAZEMBE YAIANDIKIA BARUA YANGA SC KUMTAKA IBRAHIM AJIBU KAMA MCHEZAJI HURU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeomba ya kuidhinishiwa kumchukua kiungo mshambuliaji wa Yanga ya Dar es Salaam, Ibrahim Ajibu Migomba kufuatia kusaini naye mkataba wa awali.
    Katibu wa TP Mazembe, Dony Kabongo amemuandikia barua Katibu wa Yanga kumtaarifu juu ya klabu yake kusaini mkataba wa awali na Ajibu na kuomba barua ya mchezaji huyo kuruhusiwa kuondoka Jangwani mkataba wake utakapomalizika Juni 30.
    Kabongo amesema TP Mazembe inataka kumsajili Ajibu kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake Yanga SC na hivyo imeomba barua ya kuruhusiwa kuondoka ili wamsajili kuanzia Julai 1 atakapokuwa huru rasmi.
    Ibrahim Ajibu amesaini mkataba wa awali kujiunga na TP Mazembe ya DRC

    Ajibu mwenye umri wa miaka 22, anaondoka Yanga SC baada ya kuitumikia kwa misimu miwili kufuatia kujiunga nayo akitokea kwa mahasimu wa jadi, Simba SC kama mchezaji huru pia. 
    Ajibu aliibukia timu ya vijana ya Simba, ambayo ilimtoa Boom FC ya Ilala mwaka 2013, kabla ya kwenda kujiunga na Mwadui FC na kuisaida kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2014-2015 kabla ya kurejeshwa Msimbazi.
    Amewahi kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa klabu ya Lamontville Golden Arrows FC ya Afrika Kusini na Haras El Hodoud ya Misri ambako kote iliripotiwa amefuzu, lakini hakuwa kujiunga nazo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TP MAZEMBE YAIANDIKIA BARUA YANGA SC KUMTAKA IBRAHIM AJIBU KAMA MCHEZAJI HURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top