• HABARI MPYA

  Wednesday, May 22, 2019

  MAKAMBO AFUNGA BAO PEKEE YANGA SC YAICHAPA MBEYA CITY 1-0 UWANJA WA UHURU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Yanga SC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Heritier Ebenezer Makambo aliyefunga dakika ya 26 akimalizia kwa kichwa mpira wa adhabu wa beki wa kushoto, Mwinyi Hajji Mngwali pembezoni mwa Uwanja wa kushoto.
  Mpira huo ulitengwa baada ya kiungo chipukizi wa Yanga SC, Gustavo Simon kuangushwa na beki wa Mbeya City pembezoni mwa Uwanja kushoto.


  Kwa ushindi huo, Yanga SC wanafikisha pointi 86 baada ya kucheza mechi 37, sasa wakizidiwa pointi tano na mabingwa tayari, Simba SC.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo,  Mwadui FC 3-0 imeichapa African Lyon Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga mabao ya Frank John dakika ya 75, Salim Aiyee dakika ya 89 na Ditram Nchimbi dakika ya 90 na ushei.
  Na bao la Yusuph Mhilu dakika ya 50 limeinusuru Ndanda FC kulala mbele ya Lipuli FC iliyotangulia kwa bao la Paul Nonga dakika ya 23, wafungaji wote wachezaji wa zamani wa Yanga SC timu hizo zikitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu unafutia Saa 2:00 usiku kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAKAMBO AFUNGA BAO PEKEE YANGA SC YAICHAPA MBEYA CITY 1-0 UWANJA WA UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top