• HABARI MPYA

  Tuesday, May 28, 2019

  STAND UNITED YASHUKA DARAJA, KAGERA SUGAR NA MWADUI FC ZAANGUKIA ‘KAPUNI’

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  TIMU ya Stand United imeipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuchapwa mabao 2-0 na JKT Tanzania 2-0 Uwanja wa Meja Isamuhyo, Mbweni mjini Dar es Salaam leo.
  Mabao yaliyoizamisha Stand United, maarufu kama Chama la Wana leo yamefungwa na Samuel  Kamuntu dakika ya 51 na Najim Magulu dakika ya 73.
  Stand United inaungana na African Lyon ya Dar es Salaam iliyoshika mkia kuipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu baada ya zaidi ya miaka 20 ya kushiriki mfululizo ligi hiyo.
  JKT Tanzania iliyorejea msimu huu Ligi Kuu, imenusurika kushuka baada ya kumaliza na pointi 47 katika nafasi ya 10, wakati Stand United imemaliza nafasi ya 19 kwa pointi zake 44. 
  Nazo Kagera Sugar ya Bukoba na Mwadui FC ya Shinyanga zitamenyana na timu za Daraja la Kwanza, Pamba SC na geita Gold kuwania kubaki Ligi Kuu katika mechi za mchujo.
  Hiyo ni baada ya Kagera Sugar kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Mbao FC jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza na Mwadui FC kushinda 3-1 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
  Mjini Mwanza Kagera Sugar walitangulia kwa bao la Ally Ramadhan dakika ya 20, kabla ya Hebert Lukindo kuisawazishia Mbao FC dakika ya 60, wakati Mtwara bao la Ndanda lilifungwa na Kigi Makasi huku ya Mwadui FC yakifungwa na Ottu Joseph mawili na Salim Aiyee moja.
  Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar inayofundishwa na Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Mecky Mexime imemaliza nafasi ya 18 kwa pointi zake 44 sawa na Stand United ilyomaliza nafasi ya 19 na Mwadui FC ya 17, zikizidiana tu wastani wa mabao. 

  MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LIGI KUU LEO
  Coastal Union 0-0 Singida United.
  Mbeya City 0-0 Biashara United.
  Mtibwa Sugar 0-0 Simba SC.
  Ruvu Shooting 1-0 Alliance FC (Fully Zullu Maganga 25’ p) . .
  JKT Tanzania 2-0 Stand United (Samweli Kamuntu 51’, Najimu Maguli 73’).
  Ndanda SC 1-3 Mwadui FC (Kigi Makasi : Ottu Joseph 39’, 41’, Salim Aiyee 61’) .
  Yanga SC 0-2 Azam FC (Daniel Amoah 45’+2, Mudathir Yahya 50’).
  Mbao FC 1-1 Kagera Sugar (Hebert Lukindo 60’ : Ally Ramadhan 20’).
  Tanzania Prisons 3-1 Lipuli FC (Benjamini Asukile 29’, Adam Adam 48’, 85’ : Seif Rashid 46’).
  African Lyon 0-2 KMC FC (Cliff Buyoya 21’, 17’)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STAND UNITED YASHUKA DARAJA, KAGERA SUGAR NA MWADUI FC ZAANGUKIA ‘KAPUNI’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top