• HABARI MPYA

  Sunday, May 12, 2019

  AUBAMEYANG AFUNGA MAWILI PIA ARSENAL YASHINDA 3-1 UGENINI

  Mshambuliaji Mgabon wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang akikimbia kushangilia baada ya kuifungia mabao mawili timu yake dakika za 52 na 63 ikiibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Burnley leo Uwanja wa Turf Moor na kumaliza nafasi ya nne kwa pointi zake 70, ikizidiwa moja na Tottenham Hotspur na mbili na Chelsea. Bao lingine la Arsenal lilifungwa na Eddie Nketiah dakika ya 90 na ushei, wakati la Burnley limefungwa na Ashley Barnes dakika ya 65 na kwa matokeo hayo Aubameyang anamaliza msimu na mabao 22 sawa na Waafrika wenzake, Mmisri Mohamed Salah na Msenegal Sadio Mane wote wa Liverpool ambao kwa pamoja ndiyo wafungaji bora wa msimu 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AUBAMEYANG AFUNGA MAWILI PIA ARSENAL YASHINDA 3-1 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top