• HABARI MPYA

  Sunday, May 12, 2019

  NI MAN CITY BINGWA TENA ENGLAND BAADA YA KUIPIGA BRIGHTON 4-1

  Wachezaji wa Manchester City wakishangilia na Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kukabidhiwa kufuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion jioni ya leo Uwanja wa The AMEX Falmer, East Sussex kwenye mchezo wao wa mwisho wa msimu. Mabao ya Man City yamefungwa na Sergio Aguero dakika ya 28, Aymeric Laporte dakika ya 38, Riyad Mahrez dakika ya 63 na Ilkay Gundogan dakika ya 72, kufuatia Glenn Murray kuanza kuifungia Brighton dakika ya 27.
  Man City inamaliza na pointi 98, moja zaidi ya Liverpool walioshika nafasi ya pili, wakati Chelsea imemaliza nafasi ya tatu na pointi zake 72, Tottenham Hotspur ya nne pointi 71, Arsenal ya tano pointi 70 na Manchester United ya sita pointi 66 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI MAN CITY BINGWA TENA ENGLAND BAADA YA KUIPIGA BRIGHTON 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top