• HABARI MPYA

  Tuesday, May 14, 2019

  MSUVA AENDELEZA MOTO WA MABAO MOROCOO DIFAA EL- JADIDA IKITOA SARE 1-1 UGENINI

  Na Mwandishi Wetu, CASABLANCA
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva jana ameifungia timu yake, Difaa Hassan El- Jadida ikitoa sare ya 1-1 na wenyeji, Chabab Rif Hoceima katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Pro Uwanja wa Mimoun Al Arsi mjini Al Hoceima.
  Msuva, mchezaji wa zamani wa Yanga SC ya Dar es Salaan alifunga bao hilo dakika ya nane ya mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, kabla ya Ibrahim Elbahraoui kuisawazishia Chabab Rif Hoceima dakika ya 32. 
  Na baada ya kufunga bao hilo, Msuva aliendelea kuwa mwiba kwenye safu ya ulinzi ya , Chabab Rif Hoceima kiasi cha kukaribia kufunga tena mara mbili kabla ya kupumzishwa akiwa hoi dakika ya 90, nafasi yake ikichukuliwa na Adnane El Ouardy.
  Simon Msuva akishangilia baada ya kuifungia Difaa Hassan El- Jadida ikitoa sare ya 1-1 na wenyeji, Chabab Rif Hoceima

  Kwa sare hiyo, Difaa Hassan El- Jadida inafikisha pointi 38 baada ya kucheza mechi 28, ikiendelea kushika nafasi ya sita, huku Chabab Rif Hoceima ikiendelea kushika mkia Botola Pro yenye timu 16 pamoja na kufikisha pointi 24 katika mchezo wa 28.  
  Kikosi cha Difaa Hassan El-Jadidi; Mohamed El Yousfi, Ayoub Benchaoui/Adil El Hasnaoui dk84, Marouane Hadhoudi, Youssef Aguerdoum El Idrissi, Bakary N'diaye, Ettayb Boukheriss, Mehdi Karnass, Mohammed Ali Bemammer, Elmostafa Chichane, Simon Msuva/ Adnane El Ouardy dk90 na Sekou Camara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA AENDELEZA MOTO WA MABAO MOROCOO DIFAA EL- JADIDA IKITOA SARE 1-1 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top