• HABARI MPYA

  Friday, May 10, 2019

  KEPA AIPELEKA CHELSEA FAINALI YA UEFA EUROPA LEAGUE

  Kipa wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga akiokoa penalti ya Goncalo Paciencia kabla ya Edin Hazard kuifungia The Blues penalti ya mwisho Uwanja wa Stamford Bridge mjini London na kutinga fainali ya UEFA Europa League kwa ushindi wa penalti 4-3 kufuatia sare ya jumla ya 2-2 ndani ya dakika zaidi ya 210 kwenye mechi mbili kali za nyumbani na ugenini. Chelsea ilitangulia kwa bao la Ruben Loftus-Cheek dakika ya 28, kabla ya Luka Jovic kuisawazishia Eintracht-Frankfurt dakika ya 49.
  Waliofunga penalti za Chelsea ni Ross Barkley, Jorginho, David Luiz na Hazard wakati Cesar Azpilicueta alikosa na za Eintracht-Frankfurt zimefungwa na Sébastien Haller, Jovic na Jonathan de Guzmán huku Martin Hinteregger na  Gonçalo Paciência wakikosa. Fainali itawakutanisha Arsenal na Chelsea Uwanja wa Bakı Olimpiya mjin Baku, Azerbaijani 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KEPA AIPELEKA CHELSEA FAINALI YA UEFA EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top