• HABARI MPYA

  Sunday, May 26, 2019

  WINGA WA AMAVUBI, SIBOMANA ALIYECHEZA HADI ULAYA AJA KUSAINI YANGA SC

  Na Canisius Kagabo, KIGALI
  WINGA wa kimataifa wa Rwanda na klabu ya Mukura Victory ya kwao, Patrick ‘Papy’ Sibomana amekwenda mjini Dar es Salaam kwa mazungumzo ya kujiunga na klabu ya Yanga.
  Kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online jana mjini hapa kwamba anakwenda Dar es Salaam kuzungumza na Yanga juu ya kujiunga na klabu hiyo na wakikubaliana atasaini.
  “Ndiyo nakwenda kumaliza mipango ya kuichezea Yanga, tutazungumza wakinipatia vile ni navyotaka nitasaini mkataba, na msimu ujao nitacheza Tanzania,”amesema.

  Patrick ‘Papy’ Sibomana anakuja Dar es Salaam kwa mazungumzo ya kujiunga na klabu ya Yanga

  Sibomana ameichezea Mukura Victory Sports tangu Desemba mwaka jana alipoachana Shakhtyor Soligorsk ya Belarus.
  Awali, Sibomana aliibukia klabu ya Isonga mwaka 2011 aliyochezea hadi mwaka 2013 alipojiunga na APR ambayo ndiyo iliyomuuza Ulaya mwaka 2017 ambako hata hivyo baada ya mwaka mmoja akarejea Rwanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WINGA WA AMAVUBI, SIBOMANA ALIYECHEZA HADI ULAYA AJA KUSAINI YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top