• HABARI MPYA

  Thursday, May 16, 2019

  KIGOGO WA TRA ALIYEKUWA MPINZANI WA KARIA UCHAGUZI WA TFF APEWA UONGOZI YANGA SC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI mpya wa Yanga SC chini ya Mwenyekiti wake, Dk. Mshindo Mbette Msolla umeteua Wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji.
  Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk. Msolla aliwataja Wajumbe hao jana kuwa ni Dk Athumani Kihamia ambaye ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Shijja Richard Shijja, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
  Shijja alikuwa mmoja wa wapinzani wa Wallace Karia katika uchaguzi uliopita wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwenye nafasi ya Urais. 
  Akizungumza na Waandishi wa Habari jana makao makuu ya klabu, Jangwani mjini Dar es Salaam, Dk. Msolla ambaye ni kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars alisema kwamba uteuzi huo unaanza mara moja.

  Shijja Richard alikuwa mpinzani wa Wallace Karia katika uchaguzi uliopita wa TFF  

  Dk Msolla alisema wamefanya uteuzi huo kutokana na mamlaka waliyonayo Kikatiba kuteua Wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji na uteuzi wa mjumbe mmoja aliyesalia utafanyika baadaye.
  Msolla alichaguliwa Januari 5, mwaka huu kuwa Mwenyekiti mpya wa Yanga SC kwa ushindi wa kishindo wa kura 1,276 dhidi ya 60 tu za Daktari mwenzake, Tiboroha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo chini ya uongozi uliopita.
  Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela aliyepata kura 1,206 akiwashinda Janneth Mbene (Mbunge)aliyepata kura 61, Titus Osoro kura 17, Yono Kevela kura 31 na Chota Chota kura 12.
  Walioshinda nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Hamad Islam aliyepata 1,206, Mhandisi Bahati Faison Mwaseba kura 1,174, Dominick Ikute kura 1,088, Kamugisha Kalokola kura 1,072, Arafat Haji kura 1,024, Salum Ruvila kura 976, Saad Khimji kura 788 na Rodgers Gumbo kura 776. 
  Uchaguzi huo ulifuatia kujiuzulu kwa viongozi wote waliongia madarakani Juni 11 mwaka 2016, Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wao, Siza Augustino Lymo, Tobias Lingalangala, Samuel Lukumay, Hussein Nyika, Omary Said Amir, Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi na Inspekta Hashim Abdallah.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIGOGO WA TRA ALIYEKUWA MPINZANI WA KARIA UCHAGUZI WA TFF APEWA UONGOZI YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top