• HABARI MPYA

  Tuesday, May 28, 2019

  AZAM FC YAMALIZA LIGI KUU KWA USHINDI, YAICHAPA YANGA 2-0 UWANJA WA TAIFA TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imemaliza vyema Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya vigogo, Yanga SC jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Pamoja na ushindi huo, Azam FC imemaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 75 nyuma ya vigogo wengine, Simba SC walioibuka mabingwa kwa pointi zao 93 na Yanga waliomaliza na pointi 86. 
  Katika mchezo wa leo, mabao ya Azam FC yamefungwa na beki wake Mghana, Daniel Amoah dakika ya 45 na ushei na kiungo Mzanzibari, Mudathir Yahya dakika ya 50.
  Ushindi huo ni sawa na kisasi kwa Azam FC baada ya kufungwa 1-0 na Yanga SC katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Uwanja wa Uhuru. 
  Wakati Simba SC ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya pili mfululizo, Stand United ya Shinyanga imeungana na African Lyon kuteremka daraja baada ya kufungwa 2-0 na JKT Tanzania. 
  Nazo Kagera Sugar ya Bukoba na Mwadui FC ya Shinyanga zitamenyana na timu za Daraja la Kwanza, Pamba SC na geita Gold kuwania kubaki Ligi Kuu katika mechi za mchujo.

  MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LIGI KUU LEO
  Coastal Union 0-0 Singida United.
  Mbeya City 0-0 Biashara United.
  Mtibwa Sugar 0-0 Simba SC.
  Ruvu Shooting 1-0 Alliance FC (Fully Zullu Maganga 25’ p) . .
  JKT Tanzania 2-0 Stand United (Samweli Kamuntu 51’, Najimu Maguli 73’).
  Ndanda SC 1-3 Mwadui FC (Kigi Makasi : Ottu Joseph 39’, 41’, Salim Aiyee 61’) .
  Yanga SC 0-2 Azam FC (Daniel Amoah 45’+2, Mudathir Yahya 50’).
  Mbao FC 1-1 Kagera Sugar (Hebert Lukindo 60’ : Ally Ramadhan 20’).
  Tanzania Prisons 3-1 Lipuli FC (Benjamini Asukile 29’, Adam Adam 48’, 85’ : Seif Rashid 46’).
  African Lyon 0-2 KMC FC (Cliff Buyoya 21’, 17’)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAMALIZA LIGI KUU KWA USHINDI, YAICHAPA YANGA 2-0 UWANJA WA TAIFA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top