• HABARI MPYA

  Monday, May 13, 2019

  SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE YA BILA KUFUNGANA NA AZAM FC LEO UHURU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Sare hiyo inayoiongezea kila timu pointi moja, inaifanya Simba SC iendelee kuongoza Ligi Kuu baada ya kufikisha pointi 82 kufuatia kucheza mechi 33.
  Simba SC sasa inawazidi watani wao wa jadi, Yanga SC kwa pointi mbili ambao hata hivyo wamecheza mechi mbili zaidi.
  Azam FC wao wanabaki nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu wakifikisha pointi 69 katika mchezo wa 36.

  Katika mchezo wa leo, Simba SC  walitawala zaidi na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini safu ya ulinzi ya Azam FC ikiongozwa na mabeki Mghana, Yakubu Mohammed na Aggrey Morris ilisimama imara kuzuia hatari zote.
  Kidogo Azam FC walifunguka kipindi cha pili na kujaribu kulitia majaribu lango la Simba, lakini mlinda mlango Aishi Manula alikuwa imara naye akilindwa na mabeki Erasto Nyoni na Yussuf Mlipili. 
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, bao pekee la Omar Ramadhani dakika ya 61 limetosha kuipa KMC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Yussuf Mlipili, Erasto Nyoni, James Kotei/John Bocco dk79, Haruna Niyonzima, Jonas Mkude, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na Clatous Chama.
  Azam FC; Razack Abalora, Nickolas Wadada, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Joseph Mahundi, Frank Domayo, Obrey Chirwa, Donald Ngoma na Ramadhan Singano/Daniel Lyanga dk53.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE YA BILA KUFUNGANA NA AZAM FC LEO UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top