• HABARI MPYA

    Thursday, May 09, 2019

    KOCHA MWINYI ZAHERA WA YANGA HATARINI KUTIWA HATIANI KWA 'UTOVU WA NIDHAMU'

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Mwinyi Zahera raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yuko hatarini kutiwa hatiani kwa makos aya kinidhamu. 
    Zahera ni miongoni mwa waliolalamikiwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kati ya viongozi, makocha na wachezaji kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 
    Walalamikiwa ni kutoka katika klabu za Ligi Kuu ya Tanzania (TPL), na Ligi Daraja la Kwanza (FDL). 

    Mbali na Zahera, makocha wengine waliolalamikiwa ni Athuman Bilal wa Stand United, Nassoro Mrisho (Geita Gold FC), na Ramadhani Nsanzurwimo (Mbeya City).
    Viongozi ni Herry 'Mzozo' Chibakasa wa Friends Rangers FC, Mohamed Hussein (Kagera Sugar FC),Walter Harrison (KMC) na Hussein Salehe wa Geita Gold FC wakati mchezaji aliyelalamikiwa ni Deus Tulusubya wa Pamba SC.
    Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itakutana Mei 12, mwaka huu mjini Dar es Salaam kujadili malalamiko hayo.
    Taarifa hiyo imetolewa na Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo alipozungumza na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA MWINYI ZAHERA WA YANGA HATARINI KUTIWA HATIANI KWA 'UTOVU WA NIDHAMU' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top