• HABARI MPYA

  Sunday, May 19, 2019

  BAYERN MUNICH YATWAA TAJI LA SABA MFULULIZO LA BUNDESLIGA

  Mats Hummels akimwagia pombe mchezaji mwenzake wa Bayern Munich, Arjen Robben kushangilia ushindi wa taji la saba mfululizo la Bundesliga baada ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt usiku wa jana Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich. Mabao ya Bayern Munich yalifungwa na Kingsley Coman dakika ya nne, David Alaba dakika ya 53, Renato Sanches dakika ya 58, Franck Ribery dakika ya 72 na Arjen Robben dakika ya 78, wakati bao pekee la Eintracht Frankfurt limefungwa na Sebastien Haller dakika ya 50.
  Kwa ushindi huo, Bayern Munich inamaliza Bundesliga na pointi 78, mbili zaidi ya Borussia Dortmund ambao jana wamemaliza na ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Borussia Monchengladbach. Robben na Ribery wanaondoka Bayern na jana wameaga 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAYERN MUNICH YATWAA TAJI LA SABA MFULULIZO LA BUNDESLIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top