• HABARI MPYA

  Saturday, May 18, 2019

  VIINGILIO VYA MECHI ZA TAIFA STARS AFCON 2019 NCHINI MISRI MWEZI UJAO HIVI HAPA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetangaza gharama za tiketi za kutazama mechi za Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inayotarajia kuanza mwezi ujao nchini Misri huku timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ikishiriki kwa mara ya pili tu kihistoria.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikishoa la Soka Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo amesema kwamba taarifa waliyotumiwa na CAF imesema kwenye michezo ya hatua ya makundi ambayo itahusisha tiketi za daraja la 1, dola 29 za Kimarekani, tiketi za daraja la 2 dola 18 na tiketi za daraja la 3 dola 6.

  Katika hatua hiyo Taifa Stars itacheza michezo yake mitatu ya Kundi C dhidi ya Senegal, Kenya na kumaliza na Algeria na kwenye hatua ya robo fainali gharama ya tiketi daraja 1 itakuwa dola 35 kwa daraja la 2 dola 24 na daraja la 3 dola 12. 
  Hatua ya nusu fainali daraja la 1 dola 59, daraja la 2 dola 29 na daraja la 3 dola 18, wakati mchezo wa mshindi wa 3 kiingilio kitakuwa dola 35 daraja la 1, dola 24 daraja la 2 na dola 12 daraja la 3.
  Mchezo wa fainali daraja la 1 dola 106,daraja la 2 dola 44 na daraja la 3 dola 24 na kwamba kwa yeyote mwenye nia ya kununua tiketi hizo za AFCON anatakiwa kuwasiliana na TFF mapema kabla ya kufungwa kwa muda wa maombi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VIINGILIO VYA MECHI ZA TAIFA STARS AFCON 2019 NCHINI MISRI MWEZI UJAO HIVI HAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top