• HABARI MPYA

    Monday, May 27, 2019

    TP MAZEMBE WAAMUA KUACHANA NA AJIBU NA SASA ANAREJEA KLABU YAKE KIPENZI, SIMBA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeamua kusitisha mpango wa kumsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Ibrahim Ajibu baada ya kushindwa kukubaliana kwenye maslahi binafsi.
    Kwa mujibu wa mawasiliano yaliyovuja baina ya Andre Mtine wa TP Mazembe na Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Frederick Mwakalebela mpango huo umekufa.
    Katiba barua yake kwa Mwakalebela ambayo pia aliwatumia nakala Mkurugenzi wa Azam TV, Patrick Kahemele, Mtine amesema wameamua kusitisha mpango huo baada ya kutofikia makubaliano na Ajibu juu ya maslahi binafsi.
    Lakini habari zaidi zinasema kwamba Ajibu ameamua kurejea klabu yake ya zamani, Simba SC kufuatia kumaliza mkataba Yanga SC mwezi huu.

    Wiki iliyopita, Katibu wa TP Mazembe, Dony Kabongo alimuandikia barua Katibu wa Yanga kumtaarifu juu ya klabu yake kusaini mkataba wa awali na Ajibu na kuomba barua ya mchezaji huyo kuruhusiwa kuondoka Jangwani mkataba wake utakapomalizika Juni 30.
    Kabongo alisema TP Mazembe inataka kumsajili Ajibu kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake Yanga SC na hivyo imeomba barua ya kuruhusiwa kuondoka ili wamsajili kuanzia Julai 1 atakapokuwa huru rasmi.  
    Ajibu mwenye umri wa miaka 22, ameitumikia Yanga SC kwa misimu miwili bila kushinda taji lolote kufuatia kujiunga nayo akitokea kwa mahasimu wa jadi, Simba SC kama mchezaji huru pia. 
    Ajibu aliibukia timu ya vijana ya Simba, ambayo ilimtoa Boom FC ya Ilala mwaka 2013, kabla ya kwenda kujiunga na Mwadui FC na kuisaida kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2014-2015 kabla ya kurejeshwa Msimbazi.
    Amewahi kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa klabu ya Lamontville Golden Arrows FC ya Afrika Kusini na Haras El Hodoud ya Misri ambako kote iliripotiwa amefuzu, lakini hakuwa kujiunga nazo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TP MAZEMBE WAAMUA KUACHANA NA AJIBU NA SASA ANAREJEA KLABU YAKE KIPENZI, SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top