• HABARI MPYA

  Saturday, May 18, 2019

  TFF KUUKAGUA UWANJA WA ILULU KAMA UKO TAYARI KWA FAINALI YA ASFC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) litafanya ukaguzi wa mwisho kwenye Uwanja wa Ilulu mjini Lindi Mei 23 mwaka huu.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo amesema ukaguzi huo ni maalum kuelekea mchezo wa fainali wa Kombe la shirikisho hilo, maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Fainali ya ASFC itafanyika Juni 1 Uwanja wa Ilulu mjini Lindi, ikizikutanisha timu za Azam FC ya Dar es Salaam na Lipuli FC ya Iringa.

  Na Ndimbo amesema katika ukaguzi huo itaangalia kama maelekezo yote yaliyotolewa yamefanyiwa kazi kama ilivyotakiwa.
  "Kufikia tarehe hiyo Uwanja unatakiwa kuwa tayari kwa mchezo wa Fainali itakayochezwa Juni 1, 2019,"amesema Ndimbo.
  Hii itakuwa mara ya pili mfululizo fainali ya ASFC kufanyika nje ya Dar es Salaam baada ya mwaka jana kufanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha ikizikutanisha Mtibwa Sugar ya Morogoro na Singida United ya Singida.
  Mtibwa Sugar ilifanikiwa kutwaa taji hilo kwa ushindi wa mabao 3-2 na msimu huu ikaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF KUUKAGUA UWANJA WA ILULU KAMA UKO TAYARI KWA FAINALI YA ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top