• HABARI MPYA

    Sunday, May 26, 2019

    AUSSEMS ASAINI MKATABA MPYA KUENDELEA KUFUNDISHA SIMBA SC HADI JULAI 2020

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mbelgiji, Patrick Winand J. Aussems amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kufundisha klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam.
    Aussems amesaini mkataba huo mpya leo mbele ya Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, mfanyabiashara bilionea Mohammed ‘Mo’ Dewji na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Swedi Nkwabi.
    Na Simba SC imeamua kumpa mkataba mpya Aussems baada ya msimu wake mzuri wa kwanza akiiwezesha klabu kutetea ubingwa kufikia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambako ilikwenda kutolewa katika Robo Fainali na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems (kushoto) akisaini mkataba nyumbani kwa Mohammed 'Mo' Dewji leo mjini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa klabu, Swedi Nkwabi.
    Patrick Aussems (kushoto) wakati wa kusaini mkataba leo nyumbani kwa Mohammed 'Mo' Dewji (kulia). Katikati ni Mwenyekiti wa klabu, Swedi Nkwabi.

    Hadi Julai 2020; Sasa Patrick Aussems (kushoto) ataendelea kufundisha Simba SC hadi mwishoni mwa msimu ujao 

    Hadi sasa, Aussems ameiongoza Simba SC katika mechi 67 za mashindano yote na za kirafiki, ikishinda 47, kufungwa 11 na sare 10.
    Pamoja na kutetea ubingwa wa Bara na kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa, pia Aussems aliiwezesha Simba SC kutwaa Ngao ya Jamii ikiifunga 2-1 Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza na kuifikisha fainali ya Kombe la Mapinduzi ambako ilifungwa 2-1 na Azam FC Uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba.
    Aussems alijiunga na Simba SC Julai mwaka jana akitokea timu ya taifa ya Nepal akichukua nafasi ya Mfaransa, Pierre Lechantre aliyeondoka mwezi Mei baada ya kutofautiana na uongozi.
    Aussems aliyezaliwa Februari 6, mwaka 1965 mjini Moelingen, Ubelgiji ana uzoefu wa kufundisha timu kadhaa Asia na Ulaya – lakini amewahi kufundisha KSA ya Cameroon na AC Leopards ya Dolisie nchini Kongo, hizo zikiwa timu pekee za Afrika.
    Aussems alianza kama mchezaji wa kwao, akichezea klabu za RCS Vise (1974–1981), Standard Liege (1981–1988), K.A.A. Gent (1988–1989), R.F.C. Seraing (1989–1990) na ES Troyes AC ya Ufaransa kuanzia mwaka 1990 hadi 1993, ambayo ilikuwa timu yake ya kwanza kufundisha akianza kama kocha mchezaji mwaka 1992.
    Mwaka 1995 alienda kufundisha SS Saint-Louisienne hadi 1999 alipohamia Capricorne Saint-Pierre hadi 2002 alipokwenda Stade Beaucairois hadi 2003 alipojiunga na Stade de Reims zote za Ufaransa hadi mwaka 2004 alipokuja Afrika kufundisha KSA ya Cameroon hadi mwaka 2006 aliporejea Ufaransa kufundisha SCO Angers.
    Timu nyingine alizofundisha ni Evian Thonon Gaillard F.C. ya Ufaransa pia kuanzia 2009 hadi 2011 alikwenda China kufundisha Shenzhen Ruby (2011) na Chengdu Blades kuanzia 2012 hadi 2013 aliporudi Afrika kufundisha AC Leopards hadi mwaka 2015 alipokwenda kufundisha timu ya taifa ya Nepal.
    REKODI YA PATRICK J AUSSEMS SIMBA SC
    1. Simba SC 1-1 F.C.E KSAIFA (ya Palestina, kirafiki ziara ya Uturuki)
    2. Simba SC 3-1 MC Oujder (ya Morocco, Kirafiki ziara ya Uturuki)
    3. Simba SC1-1 Asante Kotoko (ya Ghana, Kirafiki Taifa)
    4. Simba SC 0-0 Namungo FC (Kirafiki Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi)
    5. Simba SC 2-1 Arusha United (Kirafiki Uwanja wa S.A. Abeid, Arusha)
    6. Simba SC 2-1 Mtibwa Sugar (Ngao ya Jamii Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza)
    7. Simba SC 1-0 Tanzania Prisons (Ligi Kuu Taifa)
    8. Simba SC 2-0 Mbeya City (Ligi Kuu Taifa)
    9. Simba SC 4-2 AFC Leopards (Kirafiki Taifa)
    10. Simba SC 0-0 Ndanda FC (Ligi Kuu Mtwara)
    11. Simba SC 0-1 Mbao FC (Ligi Kuu Mwanza)
    12. Simba SC 3-1 Mwadui FC (Ligi Kuu Shinyanga)
    13. Simba SC 0-0 Yanga SC (Ligi Kuu Taifa)
    14. Simba SC 2-1 African Lyon (Ligi Kuu Taifa)
    15. Simba SC 3-0 Stand United (Ligi Kuu Taifa)
    16. Simba SC 5-1 Alliance FC (Ligi Kuu Taifa)
    17. Simba SC 5-0 Ruvu Shooting FC (Ligi Kuu Taifa)
    18. Simba SC 2-0 JKT Tanzania (Ligi Kuu Mkwakwani)
    19. Simba SC 0-0 Big Bullets (Kirafiki Uwanja wa Taifa)
    20. Simba SC 0-0 Lipuli FC (Ligi Kuu Uwanja wa Taifa)
    21. Simba SC 4-1 Mbabane Swallows (Ligi ya Mabingwa Afrika Taifa)
    22. Simba SC 4-0 Mbabane Swallows (Ligi ya Mabingwa Afrika Manzini) 
    23. Simba SC 1-2 Nkana FC (Ligi ya Mabingwa Afrika Kitwe) 
    24. Simba SC 2-1 KMC (Ligi Kuu Uwanja wa Taifa)
    25. Simba SC 3-1 Nkana FC (Ligi ya Mabingwa Afrika Taifa) 
    26. Simba SC 3-0 Singida United (Ligi Kuu Uwanja wa Taifa)
    27. Simba SC 4-1 Chipukizi United (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    28. Simba SC 1-0 KMKM (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    29. Simba SC 1-0 Mlandege (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    30. Simba SC 0-0 (3-1 penalti) Malindi (Kombe la Mapinduzi, alikuwa Dar na timu A)
    31. Simba SC 3-0 JS Saoura (Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Taifa)
    32. Simba SC 1-2 Azam FC (Alibaki Dar, Fainali Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    33. Simba SC 0-5 AS Vita (Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Kinshasa)
    34. Simba SC 2-1 AFC Leopards (SportPesa Super Cup Taifa)
    35. Simba SC 1-2 Bandari FC (SportPesa Super Cup Taifa)
    36. Simba SC 0-0 (Penalti 5-3) Mbao FC (SportPesa Super Cup Taifa)
    37. Simba SC 0-5 Al Ahly (Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Cairo)
    38. Simba SC 3-0 Mwadui FC (Ligi Kuu Taifa)
    39. Simba SC 1-0 Al Ahly (Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Dar)
    40. Simba SC 1-0 Simba SC (Ligi Kuu Taifa)
    41. Simba SC 3-0 African Lyon (Ligi Kuu Sheikh Amri Abeid)
    42. Simba SC 3-1 Azam FC (Ligi Kuu Taifa)
    43. Simba SC 3-1 Lipuli FC (Ligi Kuu Samora)
    44. Simba SC 2-0 Stand United (Ligi Kuu Kambarage)
    45. Simba SC 0-2 JS Saoura (Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Bechar)
    46. Simba SC 2-1 AS Vita (Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Dar)
    47. Simba SC 2-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Taifa)
    48. Simba SC 2-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Taifa)
    49. Simba SC 3-0 Mbao FC (Ligi Kuu Taifa)
    50. Simba SC 0-0 TP Mazembe (Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika Dar)
    51. Simba SC 1-4 TP Mazembe (Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika Lubumbashi)
    52. Simba SC 2-1 Coastal Union (Ligi Kuu Mkwakwani, Tanga)
    53. Simba SC 1-2 Kagera Sugar (Ligi Kuu Kaitaba, Bukoba)
    54. Simba SC 2-0 Alliance FC (Ligi Kuu Kirumba, Mwanza)
    55. Simba SC 2-1 KMC (Ligi Kuu Kirumba, Mwanza)
    56. Simba SC 2-0 Biashara United (Ligi Kuu Musoma, Mara)
    57. Simba SC 1-0 JKT Tanzania (Ligi Kuu, Uhuru)
    58. Simba SC 2-1 Mbeya City (Ligi Kuu, Sokoine)
    59. Simba SC 1-0 Tanzania Prisons (Ligi Kuu, Sokoine)
    60. Simba SC 8-1 Coastal Union (Ligi Kuu, Uhuru)
    61. Simba SC 0-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu, Uhuru)
    62. Simba SC 0-0 Azam FC (Ligi Kuu, Uhuru)
    63. Simba SC 3-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu, Uhuru)
    64. Simba SC 2-0 Ndanda FC (Ligi Kuu, Uhuru)
    65. Simba SC 2-0 Singida United (Ligi Kuu, Namfua)
    66. Simba SC 4-5 Sevilla (Kirafiki Taifa)

    67. Simba SC 1-1 Biashara United (Ligi Kuu Taifa)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AUSSEMS ASAINI MKATABA MPYA KUENDELEA KUFUNDISHA SIMBA SC HADI JULAI 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top